Jumapili 27 Aprili 2025 - 06:42
Kuanzia tarehe 15 hadi 25 Shawwal zimeitwa "siku kumi za Baqī'"

Kikao cha kimataifa kilicho fanyika mtandaoni kiliandaliwa na Taasisi ya Baqī' ya Chicago kwa kushirikisha maulamaa mashuhuri kutoka nchi mbalimbali.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kikao hiki cha kimataifa cha mtandaoni cha Taasisi ya Baqī' ya Chicago kilifanyika kwa ushiriki wa maulamaa mashuhuri kutoka India, Iran, Marekani, Norway na Tanzania, ambapo washiriki walitoa wito wa kufanyiwa haraka ujenzi upya wa makaburi matukufu ya Ahlul-Bayt (a.s) katika makaburi ya Jannatul-Baqī'.

Hujjatul-Islam Sayyid Mahbub Mahdi Abidi, mkuu wa Taasisi ya Baqī' ya Chicago, katika hotuba yake ya ufunguzi, akizungumzia mafanikio ya maandamano ya kimataifa dhidi ya uharibifu wa Baqī', alieleza kuwa: Ushindi huu ni wa Waumini wote, kwani suala hili ni maumivu ya pamoja kwa wapenzi wote wa Ahlul-Bayt.

Akaongeza kwa kusisitiza kuwa: Mwaka ujao utakua ni kumbukumbu ya miaka mia moja tangu kubomolewa kwa Baqī', na hivyo basi tunapaswa kuanza maandalizi kuanzia sasa kwa ajili ya maandamano ya kihistoria kote duniani.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha